Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 03.12.2017

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Rose

Tottenham watamuuza mlinzi wa England Danny Rose, 27, kwenda Manchester United mwezi Januari lakini ikiwa watapewa kitita cha pauni milioni 45. (Daily Star Sunday)

Meneja mpya wa Everton Sam Allardyce anapanga kumununua mchezaji wa safu ya kati wa Sevilla na Ufaransa Steven N'Zonzi, 27. (Mail on Sunday)

Manchester United hawana mpango wa kulipa pauni miloni 100 kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 28 na badala yake wameweka thamani mchezaji huyo kuwa kati ya paunia milioni 50 na 60. (Sunday Mirror)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Gareth Bale

Chlesea wanasema afadhali wamuachilia kipa raia wa Ubelgijia Thibaut Courtois, 25, aondoke wakati mktaba wake utakamilika mwishoni mwa msimu mwaka 2019 badala ya kumuuza kwa Real Madrid mwisho wa msimu huu.

Manchaster Unites hawajakufa moto wa kumsaini mlinzi na West Brom na Northern Ireland Jonny Evans, 29, baada ya majaribio mawili kushindikana. (Sunday Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mohamed Salah

Kocha wa Misri Hector Cuper anadai kuwa Real Madrid wanammezea mate mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 25. (ON Sport TV - Egypt, via Evening Standard)

Manchester United wamajiunga na Arsenal na Barcelona kumwinda mchezaji wa safu ya kati wa Schalke na Ujerumani Leon Goretzka, 22, msimu uajo (Mail on Sunday)