Ukungu wasimamisha mechi ya kriketi kati India na Sri Lanka mjini Delhi

Sri Lanka captain Dinesh Chandimal wearing a mask while fielding against India in Delhi Haki miliki ya picha Sky Sports
Image caption Ukungu wasimamisha mechi ya kriketi kati India na Sri Lanka mjini Delhi

Ukungu na moshi katika mji mkuu wa India, Delhi, umesimamisha mechi ya Test ya kriketi, baina ya India na Sri Lanka, baada ya malalamiko ya timu ya Sri Lanka.

Mji huo mkuu wa India umekumbwa na tatizo la ukungu wa wiki kadhaa

Katika kile ambacho vyombo vya habari vya India vinasema, kitu hakikupata kutokea, baadhi ya wachezaji wa Sri Lanka walifunika nyuso uwanjani, na kulazimisha mechi kusimamishwa mara tatu, wakilalamika juu ya ukungu.

Wakati mmoja kikosi cha Sri Lanka kiliomba ushauri wa madaktari kabla ya kuendelea kucheza.

Mada zinazohusiana