Jordan yaionya Marekani ikiitaka isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

The Israeli flag flutters in front of the Dome of the Rock mosque and the city of Jerusalem, on December 1, 2017. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jordan yaitaka Marekani isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

Ayman Safadi alisema alimuambia waziri wa mashauri wa nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson kuwa hatua kama hiyo inaweza kuzua ghadhabu kubwa kwa nchi za kiarabu na ulimwengu wa kiisalmu.

Kuna uvumi kuwa Rais Donald Trump atatangaza hilo hivi karibuni na kutimiza ahadi yake aliyotoa wakati wa kampeni.

Jared Kushner, mkwe wa Trump alisema kuwa bado hakuna uamuzi uliofanywa.

Ubalozi wa Marekani kuhamia Jerusalem?

Palestina: Uhamisho wa ubalozi utaathiri amani

Katika mtandao wa Twitter, Bw Safadi alisema: #Nilizungumza na waziri Rex Tillerson kuhusu hatari ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Hatua kama hiyo inaweza kusababisha ghadhabu kwenye nchi za kiarabu na kwa ulimwengi wa kiislamu na kuzua misukosuko na pia kuhujumu jitihada za amani."

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kuna uvumi kuwa Rais Donald Trump atatangaza hilo hivi karibuni na kutimiza ahadi yake aliyotoa wakati wa kampeni.

Hakuna jibu lolote kutoka kwa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani.

Naye rais wa Palestina Mahmoud Abbas anajaribu kupata uungwaji mkono wa kimataifa katika kumshawishi Trump asifanye tangazo kama hilo.

Ofisi yake ilisema kwa aliwapigia simu Jumapili viongozi wa dunia wakiwemo rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Shimo la sungura, lafichua hekalu la miaka 700

Askofu aliyewapatia silaha Wapalestina dhidi ya Israel afariki

"Alitaka kulezea harari za uamuzi wowote wa kuhamisha ubalozo wa Marekani kwenda Jerusalem au kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Isael," mshauri wa Bw. Abbas, Majdi al-Khalidi aliliambia shirika la AFP.Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Jardan ameonya Marekani kuhusu hatari ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Mada zinazohusiana