Marekani na Korea Kusini wafanya mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi

Marekani na Korea Kusini kwenye mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Marekani na Korea Kusini kwenye mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi

Marekani na Korea Kusini wameanza mazoezi makubwa zaidi ya pamoja ya kijeshi kuwai kufanywa kati ya mataiafa hayo mawili.

Miongoni mwa ndege 230 za vita zinazoshiriki kwenye mazoezi hayo ya kila mwaka kuna ndege sita za jeshi aiana ya F-22 Raptor stealth fighters

Hii inafanyika wiki moja baada ya Korea Kaskazini kulifanyia majaribio kombora la masafa marefu kinyume na vikwazo vya Umoja wa mataifa

Jeshi la Marekani lilisema kuwa zoezi hilo la pamoja ni la kuhakikisha kuwepo amani na usalama katika rasi ya Korea.

Mada zinazohusiana