Wahudumu wa ndege waliona kombora la Korea Kaskazini likipaa

This photo taken on 29 November 2017 and released on November 30, 2017 by North Korea's official Korean Central News Agency (KCNA) shows launching of the Hwasong-15 missile which is capable of reaching all parts of the US. Haki miliki ya picha AFP/KCNA
Image caption Wahudumu wa ndege waliona kombora la Korea Kaskazini likipaa

Wahudumu kwenye ndege ya shirika la Cathay Pacific iliyokuwa katika anga ya Japan waliripoti kuona Kombora la Korea Kaskazini lililokuwa likifanyiwa majaribio wiki iliyopita.

Shirika hilo lilithibitisha kwa BBC kuwa wahudumu wa ndege waliona kitu ambacho kilikisiwa kuwa kombora hilo likiingia kwenye anga ya dunia.

Tarehe 29 mwezi Novemba Korea Kaskazini ililifanyia jaribio kombora la masafa marefu ambalo ilisema kuwa linaweza kufika popote pale nchini Marekani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wahudumu wa ndege waliona kombora la Korea Kaskazini likipaa

Jaribio hilo lilizua msukosuko zaidi na Korea Kaskazini na pia Marekani, ambao Jumatatu walianzisha mazoezi yao makubwa zaidi ya angani kuwai kufanya, ambayo yametajwa na Korea Kaskazini kuwa uchokozi.

Kombora hilo lililotajwa na Korea Kaskazini kuwa lenye nguvu zaidi lilianguka katika maji ya Japan lakini likapaa mbali zaidi kuliko kombora lolote kuwai kufanyiwa majaribio.

Kinyume na nchi zingine Korea Kaskazini mara nyingi haitangazi ikifanyia majaribio makombora yake na na wala haitoi tahadhari na njia mbayo hupitia mara nyingi hajulikani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mazoezi hayo yanashirikisha ndege 230 zikiwemo ndege hii aiana ya F-22 Raptor stealth jets na maelfu ya wanajeshi

Pyongyang haina uwezo wa kupata data ya safari za angani ili ipate kuelewa kabla ya kufanya jaribio lolote la kombora.

Mazoezi hayo ya pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini yatadumu kwa muda wa miaka mitano.

Yanashirikisha ndege 230 zikiwemo ndege aiana ya F-22 Raptor stealth jets na maelfu ya wanajeshi.

Mada zinazohusiana