Mwigizaji nyota wa Bollywood Shashi Kapoor afariki dunia

Shashi Kapoor in his younger days Haki miliki ya picha BBC Hindi
Image caption Shashi Kapoor aliigiza kwenye filamu zaidi ya 150

Mwigizaji mkongwe wa Bollywood Shashi Kapoor amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.

Kapoor, aliyeigiza katika filamu maarufu kutoka India kama vile Deewar na Kabhie Kabhie, amekuwa akiuguza kwa muda na alikuwa amelazwa hospitali.

Shashi anatoka familia ya Kapoor ambayo imetawala tasnia ya filamu za Kihindi kwa miongo mingi.

Alishinda tuzo nyingi za filamu za taifa na alitunukiwa tuzo kuu ya heshima inayopewa raia na serikali ya India mwaka 2011, tuzo ya Padma Bhushan.

Aliigiza pia katika filamu kadha za Uingereza na Marekani.

Kapoor amefariki akitibiwa katika hospitali ya Kokilaben Dhirubhai Ambani mjini Mumbai.

Mpwa wake Randhir Kapoor ameambia Press Trust of India kwamba Kapoor amekuwa akitatizwa na figo kwa miaka mingi.

Image caption Shashi Kapoor alipokuwa kijana bado

Mwili wake utazikwa kesho asubuhi.

Alikuwa amemuoa mwigizaji mwingereza Jennifer Kendal, ambaye kwa pamoja walianzisha ukumbi maarufu wa sanaa Mumbai wa Prithvi mwaka 1978.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii