Licha ya uchumi mbaya,Sudan Kusini yatumia 'drones'

drones Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kamera za usalama katika ndege ndogo zisizo na rubani

Sudani Kusini imeanzisha matumizi ya Kamera za usalama pamoja na ndege ndogo zisizo na rubani yaani'drones' ili kupambana na uhalifu katika mji mkuu Juba.

Viongozi katika nchi hiyo iliyoyumba kifedha wanasema wametumia mamilioni ya dola katika mradi huo. Mitambo hiyo itaongozwa na kampuni ya Israeli mpaka hapo wasudani wenyewe watakapoelimishwa jinsi ya kuitumia.

Sudani Kusini iliyopata uhuru miaka sita iliyopita imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka minne iliyopita. Huku viongozi wa serikali mara kwa mara wanalaumiwa kwa rushwa.

Mada zinazohusiana