Onyo jipya kuhusu Trump kuutambua mji wa Jerusalem latolewa

The Israeli flag flutters in front of the Dome of the Rock mosque and the city of Jerusalem, on December 1, 2017. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Onyo jipya kuhusu Trump kuutambua mji wa Jerusalem latolewa

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemuambia Donald Trump kuwa ana wasiwasi kuwa rais huyo wa Marekani anaweza kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Uamuzi wowote kuwa mji huo unastahili kuwa katika viwango vya mazungumzo kati ya Israel na Palestina, Bw Macron alisema.

Mapema onyo kama hilo lilitolewa na nchi za kiarabu na mataifa ya kiislamu.

Ripoti zinasema kuwa rais wa Mareknia atautambua mji wa Jerusalem kuwa mji wa mkuu wa Israel.

Israel na Palestina wote wanadai kuwa mji huo ni mji wao mkuu.

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Rais Macron alimpigia Trump simu kuelezea wasi wasi wake

Ikulu ya White House iliseam kuwa anaweza kukosa siku ya mwisho ya Jumamosi kuweka sahhihi agizo la kuzuia kuhamishwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Avivi kwenda Jerusalem.

Kila rais akiwemo Trump ametia sahhihi agizo kila baada ya miezi sita tangu bunge le Congress lipitishe mswada mwaka 1995 wa kutaka ubalozi huo kumamsihwa,

Hali ya mji wa Jerusalem ndio channzo cha mzozo kati ya Israel na Palestina wanaoungwa mkono na nchi za kiarabu na ulimwengu wa kiislamu.

Mada zinazohusiana