Mahakama kusikiliza kesi ya wapenzi wa jinsia moja walionyimwa keki Marekani

David Mullins (left) and Charlie Craig. Photo: 28 November 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption David Mullins (kushoto) and Charlie Craig walikuwa wanataka keki kwa harusi yao

Mahakama ya juu zaidi nchini Marekani itasikiliza kesi ambapo wapenzi wa jinsia moja walifukuzwa kutoka duka moja la kuoka mikate huko Colorado wakati walijaribu kununua keki ya harusi.

Mwaka 2012 muoka mikate Jack Phillips alikataa kuwaokea keki David Mullins and Charlie Craig akisema kuwa ilikuwa kinyume na imani yake kama mkiristo.

Wawili hao walipeleka kesi katika mahakama ya Colorado na mahakama kusema kuwa muoka mikate aliwabagua.

Muoka mikate anasema kuwa hiyo inakiuka haki yake ya uhuru wa dini na uhuru wa kuongea.

Wapenzi hao baadaye wakapeleka malalamishi yao kwa tume ya haki za raia huko Colorado.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jack Phillips anasema kuwa hastahili kulazimishwa kuoka keki yenye umbo na ujumbe ambao yeye mwenyewe anapinga.

Colorado imepiga biashara marufuku ya kuwabagua wataja kwa misingi ya rangi na jinsia.

Mwaka 2015 mahakama ya rufaa ya Colorado ilidumissha umuzi huu nayo mahakama ya juu ya jimbo hilo ikikataa kuisikiliza upya kesi hiyo.

Kisha Bw Phillips akaamua kupeleka kesi kwa mahakama ya juu zaidi nchini Marekani.

Anasema kuwa hastahili kulazimishwa kuoka keki yenye umbo na ujumbe ambao yeye mwenyewe anapinga.

Mawakili wake pia wanasema kuwa hakukiuka sheria zinazopiga marufuku ubaguzi kwa sababu hakuwafukuza wapenzi hao kutoka kwa duka lake na hakukataa kuwahudumia.