Afisa wa Umoja wa Mataifa afanya ziara nadra Korea Kaskazini

UN under secretary general for political affairs Jeffrey Feltman, attends a press conference in Bogota on 15 November 2017 Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Bw Feltman anatarajiwa kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un

Afisa wa masuala ya siasa wa umoja wa Mataifa anaanza ziara isiyo ya kawaida wa siku nne huko Pyongyang siku ya Jumanne

Ziara hiyo ya Jeffrey Feltman ndiyo ya kwanza kufanywa na afisa wa cheo cha juu wa Umoja wa Mataifa katika kipindi cha miaka sita.

Korea Kaskazini ilikuwa imetoa mwalika kwa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba kufanya ziara.

Ziara hii inakuja baada ya jaribio la wiki iliyopita ambalo Korea kaskazini ilidai kuwa ndilo lenye nguvu zaidi la masafa marefu ikidai kuwa linaweza kushambulia Marekani.

Bw. Feltman, mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani na afisa wa cheo cha juu zaidi kufanya kazi na Umoja wa Mataifa atakuwa mjini Pyongyang hadi Ijumaa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marekani imepeleka ndeye za aini hii za F-22 fighter jets kushiriki kwennye mazoezi na Korea Kusini

Ziara yake inakuja wakati Korea Kusini na Marekani wanafanya mazoezi makubwa zaidi ya agani kuwai kufanywa.

China ambayo ni mshirika wa jadi wa Korea Kaskazini na mshirika mkubw wa kibiashara ilimtuma mwanadiplomasia wa cheo cha juu kwenda Korea Kaskazini mwezi uliopita kwa majadiliano na maafisa huko.

Korea Kaskazini: Tutatumia ''silaha kali'' kujilinda dhidi ya Marekani

Umoja wa Mataifa unasema kuwa hakuna mipango kwa sasa kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye amejitolea kuwa mpatanishi kwenye mzozo wa Korea Kaskazini kuzuru nchi hiyo.

Mada zinazohusiana