Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 06.12.2017

Lionel Messi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lionel Messi

Lionel Messi amekataa ofa ya pauni 850,000 kwa wiki kutoka Manchester City kabla ya kusaini mkataba mpya na Barcelona. (Marca )

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kuwa hana uhakika ikiwa mchezaji wa kiungo cha kati Philippe Coutinho bado atakuwa Anfield baada ya mwezi Januari. Barcelona ilitoa ofa mara tatu kwa raia huyo wa Brazil msimu huu. (Daily Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pep Guardiola

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola atarudi na ofa kubwa ya kumsaini mshambuliaji wa Arsenal na Chile Alexis Sanchez, 28, mwezi Januari. (Independent)

Everton wamewaulizia Arsenal kuhusu mshambuliaji Theo Walcott, 28, ambaye badoa hajaanza kucheza msimu huu. (Daily Mail)

Chelsea wamepewa matumaini baada ya taarifa kuwa mlinzi wa Brazil Alex Sandro, 26, anataka kuhama Juventus. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alex Sandro

West Ham wataanza tena kumwinda mchezaji wa kiungo cha kati wa Sporting Lisbon William Carvalho, 25, (Sun)

Ivan Perisic, 28, aliyetafutwa na Manchester United majira ya joto amefichua kuwa kocha wa Inter Milan Luciano Spalletti alimshawishi asalie Italia badala ya kuhamia Old Trafford. (Mediaset kupitia Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ivan Perisic

Manchester United waliwatuma maajenti kumtazama mchezaji wa kiungo cha kati wa Lazio Sergej-Milinkovic Savic, 22, wakati wa ushindi wa 2-1 dhidi ya Sampdoria wekendi iliyopita. (Sun)

Southampton, Newcastle United na Crystal Palace wanammezea mate mlinzi wa Dandee Jack Hendry, 22. (Daily Mail)

Mada zinazohusiana