Saudi Arabia yalaani hatua ya Trump kuutambua Jerusalem kuwa mji mku wa Israel

US President Donald Trump delivers a statement on Jerusalem from the Diplomatic Reception Room of the White House in Washington, DC on December 6, 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Donald Trump

Saudi Arabia imelaani hatua ya Marekani ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel huku pia shutuma zikizidi kuongezeka kufuatia hatua hiyo.

Katika taarifa, taifa hilo la ghuba lilisema kuwa tangazo hilo la Trump sio la haki.

Lakini waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alilitaja tangazo hilo kuwa la kihistoria.

Hatua hiyo ya Ttrump ilibadilisha sera za miongo kadha za Marekani.

Hatma ya mji wa Jerusalem ni moja masuala makuu kwenye mzozo katika ya Israel na Palestina.

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Wapalestina walichoma picha za Trump

Mataifa 8 kati ya 15 ambayo kwa sasa ni wanachama wa baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa yametaka shirika hilo kufanya mkutano wa dharura kufuatia uamuzi huo wa Marekani.

Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ni jambo ambalo halijatambuliwa kimataifa na hadi sasa nchi zote zimeweka balozi zao kweny mji wa Tel Aviv.

Jerusalem una semue takatifu kwa dini tatu za kiyahudi, kiislamu na kikristo.

Image caption Ramani ya Jerusalem