Mchoro wa Yesu uliouzwa dola milioni 450 waelekea Abu Dhabi

Salvator Mundi Haki miliki ya picha Christie's
Image caption Mchoro huo unaofahamika kama Salvator Mundi au (mkomboi wa dunia) - uliuzwa mjini New York kwa dola milioni 450.

Mchoro wa miaka 500 wa Yesu ambao unaaminiwa kuwa wa Leonardo da Vinci, unapelekwa katika makavazi ya Louvre huko Abu Dhabi,

Vyombo vya habari vinasema kuwa mchoro huo ulinunuliwa na mwanamfalme nchini Saudi Arabia.

Mchoro huo unaofahamika kama Salvator Mundi au (mkomboi wa dunia) - uliuzwa mjini New York kwa dola milioni 450.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mnunuzi wake alishiriki kwenye mnada kwa njia ya simu katika mnada uliodumu kwa takriban dakika 20.

Ndio mchoro uliouzwa pesa nyingi zaidi katika historia.

Mnunuzi wake alishiriki kwenye mnada kwa njia ya simu katika mnada uliodumu kwa takriban dakika 20.

Gazeti la The New York Times liliripoti kuwa ulinunuliwa na Bader bin Abdullah bin Mohammed bin Farhan al-Saud.

Leonardo da Vinci alifariki mwaka 1519 na kuna chini ya michoro yake 20 iliyojulikana hidi sasa