Watu zaidi ya 30 wajeruhiwa Palestina makabiliano kuhusu Jerusalem

Vurugu zimeendelea huko ukanda wa gaza
Image caption Vurugu zimeendelea huko ukanda wa gaza

Vurugu zimeendelea Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi ambapo zaidi ya Wapalestina 30 wamejeruhiwa katika makabiliano na polisi wa Israel

Hii ni kufuatia hatua ya Rais Donald Trump kutangaza kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Wakati huo huo Marekani imeionya Palestina dhidi ya maamuzi yake kutotaka kukutana na makamu wa rais marekani Mike Pence katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika mapema mwezi huu.

Waandamanaji wamechoma matairi na kurusha mawe huku maafisa usalama wa Israel wakifyatulia wandamaanaji hao hewa ya kutoa machozi na risasi za mpira.

Image caption Israel wakifyatulia wandamaanaji hao hewa ya kutoa machozi na risasi za mpira

Huko Gaza kundi la kiislamu la Hamas limeitisha intifada au mapambano. Omary Shakir mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch katika eneo la Isreal na Palestina yupo mjini Ramala.

Ameiambia BBC kuwea baada ya Israel kuwepo katika eneo hilo kwa miongo kadhaa sasa Wapalestina wengi wamekuwa na hasira na tangazo la Rais Trump.

Kwa upande wake Naibu waziri anayehusika na masuala ya Diplomasia wa Israel Michael Oren ameimbia BBC kuwa tangazo la Rais Trump limeleifanya iwe siku ya furaha kwa kwa taifa la Israel na aIsrael ilitarajia vurugu kutoka kwa wapalestina.

Vurugu zaidi zinatarajiwa kuendelea hivi leo.

Wengi wa washirika wa Marekani wamejitenga na hatua hiyo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Nchi za Kiarabu wanatarajiwa kukutana siku chache zijazo kuamua hatua ya kuchukua.

Kuna wasiwasi kwamba tangazo hilo la Trump huenda likachangia kuzuka kwa wimbi jipya la ghasia.

Kundi la Kiislamu la Wapalestina la Hamas limetangaza intifada mpya, au maasi.

Kwa nini Trump akafanya hivyo?

Rais Trump alisema Jumatano kwamba "ameamua ni wakati mwafaka kutambua rasmi Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel."

"Nimeamua hatua hii itakuwa ndiyo bora zaidi kwa maslahi ya Marekani katika juhudi za kutafuta amani kati ya Waisraeli na Wapalestina," alisema.

Alisema ameiagiza wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuanza kuuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem.

Licha ya onyo kwamba hatua kama hiyo inaweza kuzua wimbi la machafuko kanda ya Mashariki ya Kati, hatua hiyo inatimiza ahadi aliyoitoa Trump wakati wa kampeni na pia kuwafurahisha wafuasi wenye msimamo mkali wa Bw Trump.

Bw Trump alisema kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ilikuwa "ni kutambua uhalisia tu," na akaongeza kwamba "ndiyo hatua ya busara kuichukua."

Bw Trump alisema Marekani itaendelea kuunga mkono suluhu ya mataifa mawili - taifa la Waisraeli na Wapalestina - mataifa yote yakiishi pamoja kwa amani.

Rais huyo pia alijizuia kurejelea msimamo wa Israel kwamba Jerusalem ni mji wake mkuu wa milele ambao hauwezi kugawanywa.

Wapalestina wanataka Jerusalem Mashariki iwe mji mkuu wa taifa la Wapalestina litakapoundwa.

Hatua imepokelewa vipi?

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel inamshukuru sana Bw Trump ambaye "amejiunganisha daima na historia ya mji mkuu huo."

Amesema Israel inawasiliana "na mataifa mengine yatakayomfuata (Trump). Sina shaka kwamba balozi nyingine zitahamia Jerusalem - wakati umefika."

Hakuyataja mataifa hayo, ingawa Ufilipino na Jamhuri ya Czech zimetajwa na vyombo vya habari Israel.

Lakini hali imekuwa tufauti upande wa Wapalestina.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wapalestina waliiharibu picha ya Donald Trump katika uwanja unaotenganisha Waisraeli na Wapalestina Bethlehem

Ismail Haniyeh, kiongozi wa Hamas, kundi linalotawala Ukanda wa Gaza, ameitisha "siku ya ghadhabu" Ijumaa na ksuema itakwua "siku ya kwanza ya intifada dhidi ya mkoloni".

"Tumetoa maagizo kwa wanachama wote wa Hamas na matawi yake yote kwua tayari kwa maagizo mapya ambayo huenda yakatolewa ya kukabiliana na hatari hii," amesema kwenye hotuba Gaza.

Hayo yakijiri, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas wa kundi la Fatah amesema wanakusudia kulalamika kupitia njia za kidiplomasia, kwa kuwasilisha malalamiko rasmi kwa Baraza al Usalama la Umoja wa Mataifa na kuitisha msimamo mkali kutoka kwa Umoja wa Mataifa ya Kiarabu.

"Tutatangaza kwamba Marekani imejiondoa kutoka kuwa mdhamini mwenza wa shughuli yoyote ile ya amani au ya kisiasa," msemaji Dkt Nasser Al-Kidwa amesema.

Mataifa ya Kiarabu na Kiislamu pia yamemshutumu Trump.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Trump "anatumbukiza kanda hiyo kwenye pete ya moto".

Viongozi wa Uingereza, Ufaransa na Ulaya pia zimetofautiana na Marekani.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema hatua ya Trump imevunja sheria za kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Kwa nini Jerusalem inazozaniwa?

Mzozo kuhusu Jerusalem ni moja ya mzozo mkubwa kati ya Israel na Wapalestina ambao wanaungwa mkono na mataifa ya Kiarabu na Kiislamu.

Mji huo una maeneo matakatifu ya dini tatu zenye kufuata imani ya Ibrahim - Uyahudi, Ukristo na Uislamu - sana maeneo mengi yanapatikana Jerusalem Mashariki.

Israel ilitwaa eneo hilo kutoka Jordan wakati wa vita kati ya nchi za Kiarabu na Israel mwaka 1967 na imekuwa ikiuchukuliwa mji wote kuwa mji wake mkuu ambao hauwezi kugawanywa.

Kwa mujibu wa maafikiano wakati wa mazungumzo ya amani ya Wapalestina na Waisraeli ya 1993, hatima ya mji huo ilifaa kuamuliwa wakati wa hatua za mwisho za mazungumzo.

Hatua ya Israel kudhibiti Jerusalem yote haijawahi kutambuliwa kimataifa na nchi zote zina afisi za kibalozi Tel Aviv.

Tangu 1967, Israel imejenga makazi kadha ya Wayahudi na kuna takriban walowezi 200,000 wa Kiyahudi eneo hilo. Makazi haya yamekuwa yakishutumiwa na jamii ya kimataifa.

Hatua ya Marekani kuitambua Israel itaonekana na baadhi kama kutilia mkazo msimamo wa Israel kwamba makazi hayo ni halali.

Mada zinazohusiana