Awaua watu wa familia kwa sumu akidai wao si "wasafi" baada ya kujiunga na dhehebu

Images of poison; bottle of poison; syringe; pills; poison symbol; another bottle Haki miliki ya picha Thinkstock; Science Photo Library
Image caption Awaua watu wa familia kwa sumu akidai wao si "wasafi"

Polisi nchini Italia wamemkamata mwanamume ambaye anadaiwa kutumia sumu ya kuua panya kuwaua watu wa familia yake kwa sababu hawakuwa "wasafi".

Mattia Del Zotto, 27, analaumiwa kwa kuweka sumu kwenye chakula cha babu na nyanya yake na cha shangazi ambao walifariki

Watu wengine watano katika familia wanaendelea kupata matibabu hospitalini.

Bw. Del Zotto alikamatwa eneo la Mozna karibu na Milan baada polisi kupata risiti kwenye kompiuta yake.

Baada ya kukamatwa alikiri kuwa alitaka kuwaadhibu watu wasio wasafi.

Mama yake aliwaambia wachunguzi kuwa hivi karibuni alikuwa amejiunga na dhehebu.

Mada zinazohusiana