Mvulana wa miaka 13 amuua mama yake na kumkata kichwa China

Map showing Wenxing in Sichuan in China
Image caption Mvulana wa miaka 13 amuua mama yake na kumkata kichwa China

Mvulana wa miaka 13 huko China amekamatwa kufuatia madai kuwa alimuua mama yake na kisha kumkata kichwa.

Mvulana huyo kisha akachukua video ya mauaji hayo na kuwatumia marafiki kupitia mtandao wa kijamii wa WeChat.

Alikamatwa siku kadhaa baadaye, baada ya rafiki yake mmoja kumuonyesha mama yake video hiyo.

Kisa hicho kilitokea katika mji wa Wenxing kwenye mkoa wa Sichuan.

Polisi walithibisha kisa hicho kwa BBC lakini hawakutoa taarifa zaidi wakisema kuwa bado kinachunguzwa.

Mvulana huyo alimuua mama yake baada ya kugombana siku ya Jumapili, iliripoti Radio Free Asia.

Kisha akamkata kichwa na kukiweka kwenye mfuko kabla ya kukitupa, kwa mujibu wa ripoti.

Mvulana huyo anaripotiwa kukamatwa akiwa shuleni.

Mada zinazohusiana