Kampuni kutumia ndege kuwafukuza wafanyakazi afisini Japan

Kampuni hiyo ya Taisei inapanga kuanza kufanyia majaribio mpango huo Aprili mwaka ujao Haki miliki ya picha Taisei
Image caption Kampuni hiyo ya Taisei inapanga kuanza kufanyia majaribio mpango huo Aprili mwaka ujao

Kampuni moja nchini Japan inapanga kutumia ndege zisizo na rubani kuwafukuza wafanyakazi wanaokosa kwenda nyumbani na kutaka kuendelea na kazi muda wao wa zamu ukimalziika.

Ndege hiyo zitakuwa zikipaa hadi walipoketi wafanyakazi wa kampuni ya Taisei na kuwachezea muziki.

Ndege hiyo maalum zitakuwa zinacheza wimbo maarufu wa Auld Lang Syne ambao mara nyingi hutumiwa kutangaza kwamba maduka au afisi zinafungwa.

Japan imekuwa ikikabiliana na tatizo lililokithiri la wafanyakazi kufanya kazi muda wa ziada kupita kiasi, tatizo ambalo limekuwa likiathiri afya ya wafanyakazi na wakati mwingine hata kusababisha vifo.

Baadhi ya wataalamu hata hivyo hawajafurahishwa na mpango huo wa Taisei na wamesema ni wazo la "kipumbavu".

Kwa mujibu wa vyombo vya habari Japan, kampuni hiyo ya huduma za usalama na usafi, itatumia ndege zilizoundwa na kampuni ya ndege zisizo na marubani ya Blue Innovation zitakazotumia teknolojia ya kampuni ya mawasiliano ya NTT East.

Image caption Wafanyakazi Japan hufanya kazi muda mwingi sana

Ndege hiyo zitakuwa na kamera na zitapaa ndani ya ofisi zikichezea wafanyakazi wahusika wimbo huo.

Taisei wanapanga kuanza mpango huo kwa majaribio Aprili 2018 na ukifanikiwa, waanze kuuzia kampuni nyingine.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii