Nguli wa miondoko ya Rock Johnny Hallyday kuagwa rasmi

Mitaa ya Ufaransa kuzizima kumuaga nguli wa muziki wa Rock Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mitaa ya Ufaransa kuzizima kumuaga nguli wa muziki wa Rock

Mamia ya raia wa Ufaransa,leo wanatarajiwa kujipanga katika mitaa ya jiji la Paris kuamuaga mwanamuziki maarufu Johnny Hallyday,aliyefariki dunia wiki hii akiwa na umri wa miaka 74.

Jeneza lake litatembezwa kwenye gari maalumu,ikifuatiwa shughuli ya mazishi ambayo itahudhuriwa pia na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye atatoa heshima zake pia kwa mwanamuziki huyo.

Bendi ya Hallyday itatumbuiza kwa kupiga ala za nyimbo zake kama sehemu ya kumbukumbu.

Mwanamuziki huyu mashuhuri amefariki siku ya jumatano kutokana na maradhi ya kansa ya mapafu.

Ibada ya mazishi yake itakayoendeshwa katika kanisa Madeleine mjini Paris inatarajiwa kufuatiliwa mubashara na idadi kubwa ya watu nchini Ufaransa