Netanyahu ziarani Ufaransa kukutana na Macron

Netanyahu ziarani Ufaransa kukutana na Macron Haki miliki ya picha EPA
Image caption Netanyahu ziarani Ufaransa kukutana na Macron

Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, anafanya ziara rasmi ya kiserikali Jijini Paris, Ufaransa leo Jumapili, kwa mazungumzo na rais wa nchi hiyo, Emmanuel Macron.

Atafanya pia mikutano kadhaa na mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Jumuia ya mataifa ya bara Ulaya-EU, kesho Jumatatu.

Katika mazungumzo yake huko Paris na Brussels, swala tata la Marekani kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli, linatazamiwa kuwa miongoni mwa ajenda kuu.

Mataifa ya EU, yamekosoa uamuzi huo wa Donald Trump kuhusu Jerusalem.

Lakini Bwana Netanyahu anasema kuwa badala ya kulaani tangazo hilo la Marekani, mataifa ya Ulaya yanafaa kuzungumzia na kulaani shambulio la roketi lililotekelezwa na Wapalestina dhidi ya Israel.

Mada zinazohusiana