Jamii ya wamaasai nchini Tanzania yapata kiongozi mpya
Huwezi kusikiliza tena

Jamii ya wamaasai wa Parakuyo nchini Tanzania imepata kiongozi mpya

Jamii ya wamaasai wa Parakuyo katika kanda ya mashariki ,nyanda za juu kusini nchini Tanzania imepata kiongozi mpya wa kimila baada ya mgogoro uliodumu kwa mwaka mmoja kati ya koo mbili za Maitei na Kamunyu zilizokuwa zikichukua nafasi iliyo achwa wazi Na chifu Tikwa Moreto aliyefariki mwanzoni mwa mwaka 2016

Chief Kashu Moreto Maitei anakuwa chifu wa sita kusimikwa na kwamba kutokana na hatua hiyo mgogoro wao sasa umekwisha ikiwa ni matokeo ya jitihahada za rais wa nne Jakaya kikwete liyeongoza mazungumzo ya usuluhishi kwa kipindi cha miezi mitano

Eagan Salla alihudhuria tukio hili la kihistoria na kutuandalia taarifa ifuatayo.