Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 11.12.2017

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Luke Shaw

Mlinzi wa Manchester United Luke Shaw anahitaji pauni milioni 5 kulipa ili kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari. NewCastle walikuwa wanamtaka mchezaji huyo wa miak 22 lakini hawakuwa wanataka kulipa pauni millioni 20 ambazo United walikuwa wanahitaji. (Sun)

United pia wamefanya mazungumzo na mchezaji wa safu ya kati Marouane Fellaini katika jaribio la kutaka asaini mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa Felliani unakamilika msimu huu. (Sun)

Gareth Bale amakubalia na na Real Madrid kuondoka klabu hiyo msimu ujao, huku Manchester United na Tottenham wakimwinda mshambuliaji huyo wa miaka 28 (Diario Gol)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gareth Bale

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa mshambuliaji Olivier Giroud, 31, atasalia klabu hiyo. Giroud amekuwa anataka kuoondoka klabu hiyo kwa mkopo. (Daily Mirror)

Juventus wanatathmini kumsaini mlinzi wa Arsenal, Hector Bellerin, 22. (Sun kupitia Tuttosport)

Mchezaji wa safu ya kati wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan anataka kuketi na meneja Jose Mourinho kujadili hatma yake katika klabu hiyo. (Daily Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sergio Romero

Arsenal wako katika nafasi nzuri ya kumsaini kipa wa Manchester United Sergio Romero, 30. (Daily Star)

Klabu ya Serie A Torino wanataka kumsaini mcheza kiungo wa kati wa Stoke Giannelli Imbula. Mchezaji huyo mwenye miaka 25 yuko kwa mkopo huko Toulouse. (Stoke Sentinel)

Aston Villa wanataka kipa wa Manchester United Sam Johnstone mkataba wa kudumu. Mchezaji huyo mwenye miaka 24 yuko kwenye mkopo na klabu hiyo. (Daily Express)

Mada zinazohusiana