Mpanda majengo marefu afariki baada ya kuanguka China

Wu Yongning uses a selfie stick to photograph himself reclining on top of a structure far above the surrounding buildings Haki miliki ya picha Weibo
Image caption Mpanda majengo marefu afariki baada ya kuanguka China

Mpanda mijengo mirefu ambaye ni maarufu sana nchini China amefariki akionyesha moja ya ujuzi wake hatari.

Wu Yongning alikuwa amejizolea maelfu ya mashabiki kwenye mtandao ya kijamii wa Weibo, kutokana na video zake fupi za kutisha akiwa juu ya majengo marefu bila ya kuchukua tahadhari zozote za kiusalama.

Wasi wasi uliwaingia mashabiki wake wakati aliacha kuchapisha video zake mwezi Novemba.

Sasa imeibuka kuwa alikufa baada ya kuanguka kutoka jumba la ghorofa 62 kwenye mji wa Changsha.

Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa alikuwa akishiriki kwenye mchezo wa kushinda pesa nyingi.

Haki miliki ya picha Weibo
Image caption Mpanda majengo marefu afariki baada ya kuanguka China