Uruguay yavunja rekodi ya kuchoma nyama nyingi zaidi duniani

A total of 16,500 kg of beef are grilled in Rodo Park in Minas, Uruguay, 120 km from Montevideo, in an attempt to break the Guinness record for "The World's Biggest Barbecue", on 10 December, 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uruguay yavunja rekodi ya kuchoma nyama duniani

Mji mdogo wa Minas nchini Uruguay umeweka rekodi kwenye kumbukumbu ya Guinness kwa kuandaa shughuli kubwa ziadi duniani ya kuchoma nyama.

Karibu wapishi 200 walitumia tani 60 za kuni kuwasha moto mkubwa ambapo tani 16.5 za nyama iliyochomwa kwa muda wa jumla ya saa 14.

Lengo lilikuwa ni kubuni rekodi ya awalia ya Argentina ambayo ilichukua rekodi kutoka Uruguay mwaka 2011.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uruguay yavunja rekodi ya kuchoma nyama duniani

Kuna ushindani mkali kati ya mataifa hayo mawili jirani kuhusu ni nani anazalisha nyama bora.

Uruguay iliyo na ng'ombe mara tatu zaidi kuliko idadi ya wakaazi wake ni moja ya wauza wakubwa wa nyama duniani.

Nyama iliyovunja rekodi ilipimwa mara mbili, kwanza ikiwa mbichi na pili baada ya kuchomwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uruguay yavunja rekodi ya kuchoma nyama duniani

Nyama iliyochomwa ilistahili kupiku ile ya tani 9.16 iliyochomwa kwenye mji wa Pampa nchini Argentina mwaka 2008.

Iliripoitiwa kuwa nyama hiyo ya Uruguay ilikuwa ya tani 10.36.

Waandalizi wanasema kuwa maelfu ya watu walikusanyika kutazama shulghuli hiyo na kula nyama.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandalizi wanasema kuwa maelfu ya watu walikusanyika kutazama shulghuli hiyo na kula nyama.

Mada zinazohusiana