Satoru Anzaki: Mfanyabiashara aandaa sherehe ya kuaga kabla ya kufa Japan

Chanzo cha picha, NHK
Satoru Anzaki akiwa kwenye karamu hiyo
Mfanyabiashara mmoja nchini Japan ambaye anaugua saratani na anatarajiwa kufariki karibuni aliwashangaza watu baada ya kuandaa karamu kubwa ya kuaga.
Satoru Anzaki aliwaalika wageni karibu 1,000 wakiwemo marafiki zake, watu waliosoma naye, washirika wake wa kibiashara na wafanyakazi wake.
Satoru, 80, ambaye ni mkuu wa zamani wa kampuni ya kuunda mashine ya Komatsu alipatikana na saratani ya kibofu cha nyongo Oktoba.
"Nimeridhika kwamba niliweza ksuema 'asante' kwa watu niliokutana nao maishani," aliwaambia wanahabari baada ya sherehe hiyo.
"Kwa kuwa nilitaka kufurahia kabisa sehemu ndogo ya maisha niliyobaki nayo, nimeamua nisipokee matibabu baada ya kuzingatia madhara ya tiba," alisema.
Alitangaza mpango wake wa kufanya sherehe hiyo kupitia tangazo gazetini, taarifa ambazo zilisambazwa sana mtandaoni watu wakitaniana kuhusu ingelikuwa wao wangewaalika nani.
Satoru alikodisha chumba katika hoteli moja Tokyo na akaipamba kwa picha za kumbukumbu ya maisha yake.

Kisiwa cha Japan ambapo wanawake hawaruhusiwi kufika
Kisiwa hicho cha Okinoshima huchukuliwa kuwa kitakatifu kaisi kwamba ni wanaume pekee wanaoruhusiwa kuzuru, gazeti la Asahi Shimbun linasema.