India Tamil Nadu: Watu sita wahukumiwa kifo kwa mauaji ya kulinda hadhi ya tabaka

CCTV footage
Image caption Picha za CCTV zilionesha tukio hilo lilivyofanyika

Watu sita wamehukumiwa kifo kwa kumuua mwanamume kutoka kwa tabaka la chini la Dalit nchini India kwa kuoa mtu ambaye hakutoka tabaka lake.

Sankar, 22, alishambuliwa mchana kwenye barabara yenye watu wengi na akafariki akikimbizwa hospitalini. Waliomuua walitoroka kwa kutumia pikipiki.

Mauaji kwa dhamira ya kulinda hadhi ya familia na tabaka nchini India ni matukio ya kawaida, lakini picha ya video zilizoonyesha kuuawa kwa Sankar zimewashangaza wengi sana nchini humo.

Mkewe Kausalya pia alijeruhiwa vibaya wakati waliposhambuliwa na watu watatu waliojihami kwa silaha kali.

Sankar alitoka tabaka la Dalit, jamii ambayo tangu jadi ilifahamika kama tabaka la chini zaidi, tabaka ambalo ndilo la chini zaidi miongoni mwa watu wa jamii ya wahindi.

Mkewe kausalya alitoka tabaka la juu.

Familia yake ilikuwa imepinga ndoa hiyo kwa misingi ya tabaka.

Babake Kausalya ni miongoni mwa wale waliohukumiwa kifo hivi leo na jaji mmoja katika jimbo la Tamil Nadu. Alijisalimisha kwa polisi baada ya kutekelezwa kwa mauaji hayo.

Kwingineko mahama nchini india imempata na hatia mtu mmoja aliyedaiwa kumbaka na kumuua mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu katika jimbo la Kerala ya Kusini, mauaji yaliyosababisha maandamano kote nchini humo.

Mwanafunzi huyo alipatikana ameuawa nyumbani kwake Aprili mwaka huu, mwili wake ukiwa na majeraha 30 ya kudungwa kwa kisu na meno.

Image caption Picha ya Kausalya akiwa hospitalini

Muhammed Ameerul Islam alihukumiwa na mahakama hiyo mjini Kerala, katika kesi ambayo imefananishwa na kesi nyingine ambapo wanaume kadhaa walihukiwa kifo kwa kumbaka na kumuua mwanafunzi mwingine mwaka wa 2012.

Islam atahukumiwa kesho na mwendesha mashtaka mkuu ameiambia mahakama kuwa bwana Islam anastahili hukumu ya kifo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii