Mshambuliaji wa New York alikuwa amemuonya Trump

Akayed Ullah, a 27-year-old Bangladeshi immigrant. Haki miliki ya picha CBS
Image caption Mshambuliaji wa New York alikuwa amemuonya Trump

Mwanamume ambaye anakabiliwia na mashtaka ya ugaidi kufuatia shambulizi la bomu kwenye kituo cha mabasi Mjini New York alimuonya rais wa Marekani Donald Trump kabla ya kufanya shambulizi hilo.

"Trump ulishindwa kulilinda taifa lako," aliandika. Onyo hilo la Akayed Ullah lilitajwa na waendesha siku ya Jumanne.

Wanasema kuwa mhamiaji huyo kutoka Bangladesh aliendesha shambulizi hilo baada ya kushawishiwa na kundi la Islamic State.

Alijijeruhi mwenyewe na watu wengine watatu siku ya Jumatatu.

Bw. Ullah analaumiwa kwa kulipua kifaa kilichokuwa kimefungwa mwilini mwake kwenye kituo cha mabasi huko Manhattan wakati wa shughuli nyingi.

Kulingana na waendesha mashtaka, Bw. Ullah alisema baada ya kukamatwa: Nilifanya hili kwa niaba ya Islamic State.

Pia aliwaambia wachunguzi kuwa alichochewa na mashambulizi ya Marekani dhidi ya maeneo ya Islamic State.

Bw. Ullah alihamia Marekani mwaka 2011 kutoka Chittagong huko Bangladesh.

Bangladesh ilisema hakuwa na historia ya uhalifu na alikuwa amezuru nchi hiyo mwezi Septemba,

Image caption Bw. Ullah analaumiwa kwa kulipua kifaa kilichokuwa kimefungwa mwilini mwake kwenye kituo cha mabasi huko Manhattan wakati wa shughuli nyingi.

Mada zinazohusiana