Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 13.12.2017

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Thomas Lemar

Chelsea wanajiandaa na ofa ya pauni milioni 80 kumsaini mchezaji wa Monaco raia wa Ufaransa Thomas Lemar, 22, ambye alikuwa pia anamezewa mate na Liverpool na Arsenal mwezi Agosti. (L'Equipe, kupitia Daily Mail)

Meneja wa West Ham David Moyes anatathmini kumsaini mchezaji wa safu ya kati wa Arsenal, Jack Wilshere, 25. (Guardian)

Mlinzi wa Juventus Alex Sandro, 26, ambaye anamezewa mate na Manchester United, amekiambia klabua hiyo ya Italia kuwa angependa kuondoka lakini angependa alekee Chelsea mwezi Januari. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Antoine Griezmann

Mchezaji ambaye amekuwa akitafwa kwa siku nyingi na Manchester Unites Antoine Griezmann, 26, anatarajiwa kuihama Atletico Madrid kwenda Barcelona msimu ujao. (Independent)

Arsenal tayari wamefikia makubaliano ya pauni milioni 35.3 kumsaini mchezaji wa Sevilla Steven Nzonzi mwezi Januari. (Gol kupitia Daily Mirror)

Pep Guardiola anaamini kuwa atahitaji kumsaini mlinzi mwezi Januari la sivyo Manchester City watakuwa matatani. (Guardian)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Thomas Meunier

Mchezaji wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 26, amehiusishwa na kuhaka kwenda Manchester United miezi ya hivi karibuni ameandika kwenye twitter kuwa angependa kuhamia Old Trafford. (Daily Express)

Wing'a wa zamani wa Everton Gerard Deulofeu, 23, ataondoka Barcelona kwenda Napoli kwa mkopo baada ya kushindwa kuwa katika kikosi cha kwanza huko Nou Camp. (Rai Sport kupitia Talksport)

Barcelona wanakaribia kukumilisha mpango wa kumsaini mlinzi wa Palmeiras raia wa Colombia Yerry Mina, 23, ambaye anaonekana kuwa atachukua mahala pake Javier Mascherano, 33. (AS)

Mada zinazohusiana