Kutafuta viumbe anga za juu: Sayari hii ndogo inapita na siri kutoka mbali?

'Oumuamua Haki miliki ya picha Eso
Image caption Mchoro wa Oumuamua

Wataalamu wanaofanya kazi katika mradi unaotafuta iwapo kuna dalili za kuwepo kwa viumbe anga za juu wanajiandaa kuchunguza sayari ndogo inayopita katika mfumo wetu wa jua kubaini iwapo kuna uwezekano wa viumbe kama hao kuwepo.

Sayari hiyo ndogo yenye umbo ambalo si kawaida kwa sayari iligunduliwa ikielekea kwenye mfumo wa jua siku ya Jumapili 19 Oktoba.

Ndiyo sayari ya kwanza kutoka kwa mfumo mmoja wa nyota iliyoingia kwenye mfumo mwingine wa nyota ambayo imetambuliwa kufikia sasa.

Sifa zake zinaonesha kwamba imetoka kwenye mfumo wa nyota nyingine.

Mpango huo ambao unaungwa mkono na bilionea Yuri Milner utatumia darubini inayotumia miali ya redio kujaribu kupata mawasiliano kutoka kwa sayari ndogo hiyo.

Juhudi za kundi hilo la wataalamu zitaanza leo Jumatano, ambapo wataalamu wa anga za juu wataitazama sayari ndogo hiyo, ambayo kwa sasa inasonga kwa kasi kuupita mfumo wetu wa jua.

Sayari ndogo hiyo itafuatiliwa kwa kutumia masafa manne tofauti ya mawimbi ya redio.

Kundi la kwanza litatazama sayari hiyo kwa kutumia darubini ya Robert C Byrd Green Bank jimbo la Virginia Magharibi kwa muda wa saa kumi.

Awali wataalamu walipoitazama sayari hiyo amabyo imepewa jina Oumuamua, waligundua ina umbo la kushangaza, ambapo ni ndefu na kuifana iwe na muonekano wa sigara.

Haki miliki ya picha NASA/JPL-Caltech/IAU
Image caption Kasi pamoja na njia inayofuatwa na sayari hiyo vinaashiria ilitoka nje ya mfumo wetu wa jua

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Darubini ya Robert C Byrd Green Bank ndiyo itatumiwa kufuatilia sayari hiyo

Jina Oumuamua maana yake ni "tarishi kutoka mbali anayefika wa kwanza" kwa lugha ya Kihawaii.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii