Israel yaendeleza mashambulizi dhidi ya Hamas kujibu mashambulizi kutoka Gaza

Israel na Hamas waendeleza mapambano kis mji wa Jerusalem
Image caption Israel na Hamas waendeleza mapambano kis mji wa Jerusalem

Jeshi la Israel limesema mashambulizi yake ya roketi yanazilenga ngome tatu za kijeshi za wapiganaji wa kundi la Hamas, ikiwa ni hatua ya kujibu shambulizi dhidi yao la kutoka ukanda wa Gaza.

Israel pia imeamuru kufungwa kwa mpaka kati yake na Gaza, baada ya shambulizi la nnela maroketi yanayodaiwa kurushwa na kundi la Hamas.

Hali hii ya mapigano ya kundi la Hamas inadaiwa kuwa ni kutokana na hasira kufuatia hatua ya rais Trump kuutambua mji wa Jesrusalem kama makao makuu ya Israel.

Hata hivyo jeshi la Israel linasema kuwa makombora kati ya yaliyorushwa, walifanikiwa kuyazuia, ambapo moja lilianguka eneo la wazi kusini mwa Israel na jingine lilipoteza mweelekeo.

Mada zinazohusiana