Mwanamume asiye na makao apata pesa nyingi uwanja wa ndege Ufaransa

People watching departure boards at Paris Charles de Gaulle airport Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanamume asiye na makao apata pesa nyingi uwanja wa ndege Ufaransa

Mwanamume ambaye alipata puani 260,000 baada ya kuegemea mlango wa kampuni ya Charkles de Gaulle kwenye uwanja wa ndege nchini Ufaransa anaaminiwa kuwa mtu asiye na makao.

Polisi wanasema kuwa walimtambua mwanamume huyo kupitia kwa kamara za cctv kama mmoja wa watu wanaolala karibu na uwanja wa ndege.

Mlango wa kampuni inayoshughulikia masuala ya fedha ya Loomis terminal 2F, ulikuwa umeachwa bila kufungwa na mwanamume ambaye umri wake unatajwa kuwa wa miaka 50 hivi alitoka nje akiwa na mifuko miwili ya pesa.

Kwa sasa anasakwa na polisi.

Mwendo wa saa (16:30 GMT) Ijumaa iliyopita king'ora kililia katika kampuni hiyo inayohusika na masuala ya fedha.

Maafisa waliochunguza video ya cctv waligundua kuwa mwananammue huyo alikuwa akitafuta kwenye ndoo za taka nje ya ofisi hizo, na kuonekaka kushangazwa wakati mlango aliokuwa ameegema ulipofunguka.

Aliingia ndani na muda mfupi baadaye akaondoka akiwa amebeba mifuko miwili.

Mwanamume huyo aliacha mfuko wake nyuma lakini haukuwa na stakabadhi yoyote ambayo ingesababisha atambuliwe.

Pesa alizochukua zinatajwa kuwa jumla ya pauni 260,000.

Mada zinazohusiana