Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 14.12.2017

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mesut Ozil

Mesut Ozil 29, angependa kuhamia Manchester United badala ya Barcelona ikiwa ataondoka Arsenal. (Daily Mail)

Ajenti wa Ozil ameimbia Barcelona kuwa ni lazima wafanye uamuzi ikiwa watamsaini mchezaji huyo au la katika kipindi cha wiki mbili zinazokuja (Mundo Deportivo)

Nahodha wa Barcelona Andres Iniesta anasema mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, atakuwa muhimu ikiwa watamuendea mwezi Januari. (Goal)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ronaldo

Ronaldo anawaomba ushauri mawakili wake kujaribu kuondoka Real Madrid. (El Chiringuito kupitia Daily Express)

Willian amewahakikishia mashabiki wa Chelsea kwamba hataondoka mwezi Januari, baada mchezaji huyo wa safu ya kati kuhusishwa na kuelekea huko Manchester United na Barcelona. (Evening Standard)

Newcastle wanatathmini kumpa ofa mshambuliaji wa Liverpool Danny Ings, 25 na mlinzi wa Manchester United Luke Shaw, 22, mwezi ujao. (Daily Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Ings

Jose Mourinho amemuorodhesha mchezaji wa safu ya kati wa Inter Milan raia wa Ureno Joao Mario, 24, kama atakayechukua mahala pake Henrikh Mkhitaryan huko Manchester United. (Corriere dello Sport kupitia Mirror)

Kipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma, 18, ametaka mkataba wake mpya kufutwa huko Real Madrid wakati Paris St-Germain wakitaka kumsaini. (Gazzetta dello Sport)

Sporting Lisbon wanataka kumchukua mshambuliaji wa Leicester Islam Slimani, 29, kutoka Ureno kwa mkopo mwezi Januari. (A Bola, kupitia Talksport)

Mada zinazohusiana