Mshambuliaji wa kujitoa mhanga awaua polisi 17 Mogadishu

File image from March 5, 2012 shows al-Shabab recruits walking down a street in the Deniile district of Somali capital, Mogadishu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Al-Shabab is fighting an insurgency against Somalia's UN-backed government

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga amewaua takriban polisi 17 wakati wa waride ya mafunzo kwenye taasisi ya kutoa mafunzo huko Mogadishu.

Takriban watu wengine 17 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Mshambuliaji huyo ambaye alidanganya kuwa afisa wa polisi alijilipua kwenye taasisi kutoa mafunzo ya polisi ya General Kaahiye.

Kundi la wanamgambo la al-Shabab linasema kuwa lilitekeleza shambulizi hilo.

Kundi hilo mara nyingi huendesha mashambulizi ya mabomu mjini Mogadishu na miji mingine.

Walioshuhudia walisema kuwa maafisa hao walikuwa wamesongamana wakielekea kwa waride yao ya asubuhi wakati mlipuaji alilipua vilipuzi vyake.

Mada zinazohusiana