Mahakama ya Juu Kenya yasema hukumu ya kifo inakiuka katiba
Huwezi kusikiliza tena

Mahakama ya Juu Kenya yasema hukumu ya kifo inakiuka katiba

Mahakama ya Juu nchini Kenya imesema hukumu ya kifo ambayo imekuwa ikitolewa na mahakama nchini humo kwa baadhi ya makosa ni kinyume cha katiba.

Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo kutokana na rufaa iliyokuwa imewasilsihwa na wafungwa wawili ambao walihukumiwa kifo.

Hadi sasa makosa makubwa nchini Kenya kama wizi wa kimabavu au mauaji yana hukumu ya kifo pekee, na sheria hazimpi hakimu au jaji nafasi ya kumfunga jela mshtakiwa.

Lakini kufuatia uamuzi huo wa Mahakama ya Juu, majaji na mahakimu watakuwa na uhuru wa kutoa hukumu nyingine badala ya hukumu ya kifo.

Hata hivyo, jaji mwenyewe anaweza kutoa hukumu ya kifo kwa mfungwa kwa hiari yake.

Ingawa hukumu ya kifo imekuwepo kwenye sheria za Kenya, taifa hilo halijawanyonga wafungwa wowote katika kipindi cha miaka 30.

Wengi wa waliohukumiwa kunyongwa huishi gerezani maisha na huishi wakiwa na wasiwasi bila kujua ni wakati gani hukumu dhidi yao inaweza kutekelezwa, jambo ambalo limeshutumiwa na makundi ya kutetea haki za kibinadamu.

Je, uamuzi huu una umuhimu gani?

Mwandishi wetu Ferdinand Omondi alifanya mahojiano na Peter Ouko, balozi wa shirika la Africa Prisons Project, aliyewahi hukumiwa kifo na kuwa mfungwa kwa miaka kumi na minane kabla ya kuachiliwa huru kwa msamaha wa rais.

Mada zinazohusiana