HRW: Polisi na wanajeshi walitenda unyanyasaji wa kingono Kenya
Huwezi kusikiliza tena

HRW: Polisi na wanajeshi walitenda unyanyasaji wa kingono wakati wa uchaguzi Kenya

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa vikosi vya usalama nchini Kenya vilitekeleza vitendo vya ukatili wa kingono wakati na baada ya uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti.

Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch linasema kuwa liliwahoji wanawake 68 na waathiriwa watatu wa ubakaji watatu katika mji mkuu Nairobi, na katika maeneo kadhaa magharibi mwa Kenya .

Wengi miongoni mwa wanawake na wasichana waliohojiwa walisema kuwa walibakwa na wanaume kadhaa, na wengi wao walikuwa ni polisi ama wanajeshi .

Mwandishi wetu Nasteha Mohamed alizungumza na waathiriwa wawili wanaoelezea masaibu yao.