Dereva aliyesababisha ajali ya gari la shule kuhojiwa Ufaransa

Ajali hiyo ilitokea karibia na eneo la shule
Image caption Ajali hiyo ilitokea karibia na eneo la shule

Wapelelezi nchini Ufaransa wanasubiria kumuhoji mwanamke dereva wa gari la shule lililogonga treni karibu na Perpignan Mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watoto wanne.

Amepata majeraha kadhaa.

Waziri mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe aliyekwenda eneo la tukio amesema watu 11 wapo katika hali mbaya.

Wengine tisa walijeruhiwa kidogo.

Amesema kazi ya kuwatambua majeruhi imekua ngumu.

Gari hilo lilikuwa ndio limepakiwa wanafunzi hao muda mfupi na lilitembea mwendo wa kilomita moja tu kabla ya ajali hiyo.