Benki kuu Nigeria yatoa fedha kupambana na Boko Haram

Kundi la Boko Haram lilianzishwa mwaka 2002
Image caption Kundi la Boko Haram lilianzishwa mwaka 2002

Gavana wa benki kuu ya Nigeria ameidhinisha kutolewa kwa dola bilioni moja kusaidia serikali kupambana na kundi la wapiganaji wa Boko Haram.

Fedha hizo zitatoka katika akaunti ya akiba ya fedha za mauzo ya mafuta.

Licha ya Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari kusema kuwa vita dhidi ya Boko Haram vinaelekea ukingoni, lakini kundi hilo limekua likiendeleza mashambulizi yake Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na nchi jirani.