Ubakaji ni janga kiasi gani kwa mataifa ya Afrika?

Mvulana Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ripoti inasema maelfu ya watoto wamebakwa

Uchunguzi wa miaka mitano nchini Australia umewasilisha ripoti ya mwisho inayosema, taasisi ''zilishindwa pakubwa'' kuwalinda watoto.

Tume maalum iliyopewa jina - The Royal Commission, imesikiza ushahidi wa kutisha kutoka kwa maelfu ya manusura kote nchini humo.

Imegundua dhulma kutoka katika taasisi elfu 4, zikiwemo za kidini, vilabu vya michezo, nyumba za kuwahudumia mayatima na kambi za kijeshi.

Taswira hii inalingana kwa kiasi gani na baadhi ya mataifa barani Afrika?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa Jamhuri ya Congo wahukumiwa maisha kwa ubakaji

DRC

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo inatazamwa kuwa mojawapo ya mataifa yenye viwango vya juu vya unyanyasaji wa kingono duniani.

Mfano mzuri wa hivi karibuni ni hivi juzi wanamgambo kadhaa katika nchi hiyo wamefungwa maisha kwa kuwabaka watoto wapatao 40, akiwemo mtoto mmoja mchanga.

Wanaharakati wa kutetea haki za binaadamu na waandishi habari waliiangazia kesi na kuileta mbele ya duniani -- katika kujaribu kushinikiza maafisa nchini Congo waidhinishe hukumu.

Wanaharakati hao wanasema hukumu hiyo sasa imekuwa pigo kwa mtindo wa kutoshtakiwa wanyanyasaji wa aina hiyo DRC -- lakini ni hatua kubwa zaidi iliyosalia kupigwa kwa jumla katika kupambana na tatizo hilo.

Haki miliki ya picha SAMER MUSCATI HUMAN RIGHTS WATCH

Uganda:

Wanawake nchini Uganda wamo katika hatari mara mbili zaidi ya wanaume kunyanyaswa kingono. Asilimia 22 ya wanawake walio na umri wa kati ya miaka 15-49 wameripoti kuwa wamenyanyaswa kimapenzi katika kiwango kimoja katika maisha yao. Utafiti wa mwaka 2016 wa shirika la data na afya ya raia Uganda, unasema.

Ndiposa kumeanzishwa jitihada za kuwasaidia wanawake na hususan wasichana wanaofanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

Kenya

Nchini Kenya 47% ya wanawake na wasichana wa kati ya umri wa miaka 15-49 wameripoti kupitia unyanyasaji wa kingono au kimwili kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2014 wa shirika la data na afya ya raia Kenya (KDHS).

Ripoti mpya ya wanaharakati wa haki za binadamu kutoka Human Rights Watch wanasema kuwa unyanyasaji wa kingono ulienea wakati na baada ya uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti 2017.

"Wanawake na wasichana waliohojiwa na HRW waliwataja baadhi ya watuhumiwa kuwa maafisa wa polisi au wanaume waliovalia sare, waliobeba bunduki, na marungu, na wengine ambao ni sungu sungu na hata raia," ripoti hiyo inasema.

Serikali ya Kenya hatahivyo imekanusha yaliomo katika ripoti hiyo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii