Dalai Lama azindua programu tumishi ya iPhone

Dalai Lama Haki miliki ya picha SANJAY BAID
Image caption App ya Dalai Lama ni ya bure

Dalai Lama amezindua programu tumishi ya simu kwa wafuasi wake kuweza kufuatilia kwa karibu kuhusu safari na mafunzo yake.

Kiongozi huyo wa kidini wa Tibet anayeishi uhamishoni mwenye umri wa miaka 82, ana akunti ya Twitter iliyo na wafuasi zaidi ya milioni 16.

App hiyo ya bure kwa sasa inapatikana kwenye simu za iPhone pekee, na ataitumia kutoa taarifa, video, picha na taarifa nyinginezo

China yaionya Botswana kuhusu Dalai Lama

Kuna programu nyinge tumishi za kidini zilizozinduliwa, zinazoruhusu viongozi kuwasiliana na wafuasi wao na kuwasiaidia watu kutafuta chakula kinachoambatana na dini zao, wanaposafiri.

App hiyo inaitwa, Dalai Lama, haijakaguliwa sana na watumizi.

The Dalai Lama

  • Jina lake ni Tenzin Gyatso
  • AlizaliwaTibet, amekuwa uhamishoni kwa miongo sita tangu Uchina ukandamize vuguvugu la Tibet
  • Yeye ni Budda, anayetambulika kama mojawapo ya viongozi wakuu duniani na huhubiri amani na uvumilivu wa ki imani mara kwa mara
  • Anashinikiza kujitawala kwa Tibet iliomo ndani ya China lakini utawala wa China unamuona kuwa mtu anayeshinikiza kugawanayika kwa nchi hiyo
  • Mnamo 1989 alishinda tuzo ya Nobel ya amani
  • BBC imeshinda kupata picha yake akiwa anatumia simu za kisasa 'smartphone'

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii