Afrika kwa Picha: 8-14 Desemba 2017

Mkusanyiko wa picha kutoka Afrika na kuhusu Waafrika wiki hii:

Sabrina Simader of Kenya in action during the women"s Slalom of the Alpine Combined race of the FIS Alpine Skiing World Cup in St. Moritz, Switzerland, 08 December 2017. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mkenya Sabrina Simader akipaa angani wakati wa mashindano ya wanawake ya slalom (mashindano ya kuteleza kwenye barafu) yaliyofanyika St Moritz, Usiwzi siku ya Ijumaa.
A Long March 3B rocket carrying Alcomsat-1, Algeria"s first telecommunications satellite, takes off at the Xichang Satellite Launch Center in Sichuan province, China December 11, 2017. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Setilaiti ya kwanza ya mawasiliano ya Algeria pia ilirushwa angani kutoka kituo cha kurushia maroketi na setilaiti cha Xichang nchini China Jumatatu.
Members of the Africa Diaspora Forum (ADF), civil society organisations, churches, trade unions and other coalitions wear chains and shout slogans during a demonstration against the slave trade and human trafficking in Libya on December 12, 2017 at the Union Buildings in Pretoria. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanaharakati mbalimbali Afrika Kusini waliandamana Jumanne baada ya taarifa kutolewa kwamba wahamiaji wanauzwa kama watumwa Libya...
Migrants stand in a detention centre run by the interior ministry of Libya"s eastern-based government, in Benghazi, Libya, December 13, 2017. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji hawa walipigwa picha katika kituo cha kuwazilia wahamiaji katika mji wa Benghazi, Libya...
Malian migrants are transferred by bus to a temporary shelter upon their arrival in Bamako on December 13, 2017, after being repatriated from Libya by the IOM (International Organisation for the Migrations). Haki miliki ya picha AFP
Image caption Na familia hii kutoka Mali ni miongoni mwa mamia ya wahamiaji ambao wamesaidia kuondoka Libya na kurudi nyumbani wiki za karibuni baada ya kusaidia kutokana na malalamiko kutoka kwa mataifa na mashirika mbalimbali kote barani baada ya taarifa za wahamiaji kuuzwa kama watumwa kutokea.
Isabel Antonio, a 16-year-old singer and refugee from the Democratic Republic of Congo, poses for a portrait at Ipanema beach in Rio de Janeiro, Brazil on December 6, 2017. She lost her country and childhood in one of Africa"s most terrible wars, but Congolese refugee Isabel Antonio has won the hearts of millions of Brazilians with her performances on The Voice Brasil. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Picha hii nayo iliyotolewa Ijumaa inamuonesha Isabel Antonio, 16, mwanamuziki na mhamiaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akipigwa picha katika ufukwe wa Ipanema jijini Rio de Janeiro, Brazil. Aliwavutia mamilioni ya watu katika kipindi cha runinga cha kutavuta watu wenye vipaji cha The Voice Brasil.
Kenyan-Mexican actress Lupita Nyong"o poses on the red carpet during the world premiere of "Star Wars: The Last Jedi" at the Shrine Auditorium in Los Angeles, California, USA, 09 December 2017. Nyong"o plays the role of Maz Kanata in the film. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Na jimbo la California, mwigizaji Mkenya-Mmexico Lupita Nyong'o anapigwa picha kwenye zulia jekundu wakati wa kuzinduliwa kwa filamu ya Star Wars: The Last Jedi Jumamosi. Nyong'o ameigiza nafasi ya Maz Kanata.
Nigerian soprano Omo Bello rehearses in Lagos on December 8, 2017. A live performance of an aria from an Italian opera, sung by a professional soprano, isn"t a common sound in Nigeria"s bustling commercial and entertainment capital. But it"s not the strangest thing for the performer, Omo Bello. News of her appearance in Lagos has attracted a crowd, even it"s only for a short rehearsal. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Barani, Omo Bello anafanya mazoezi ya uimbaji Lagos. Mtindo wa uimbaji wa Opera si maarufu sana Nigeria lakini AFP wanasema watu wengi walikusanyika kumsikiliza akifanya mazoezi.
A woman shows how to use female condoms at a stand on December 8, 2017 in Abidjan, as part of the 19th ICASA conference (International Conference on AIDS and STIs in Africa). Haki miliki ya picha AFP
Image caption Na IJumaa, mwanamke anaonesha watu jinsi ya kutumia kondomu ya wanawake katika mkutano wa kimataifa wa 19 wa vita dhidi ya Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa Afrika (Icasa) katika mji wa Abidjan nchini Ivory Coast.
A stone sculptor at work along the highway to the Robert Mugabe International airport, Harare, Zimbabwe, 12 December 2017. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mchongaji sanamu huyu naye anapangusa sanamu zake anazoziuza Harare siku ya Jumanne. Yeye ni miongoni mwa mamilioni ya raia wa Zimbabwe wanaotumai kwamba bishara zao zitaimarika chini ya Rais Emmerson Mnangagwa. Sanamu hizo na vinyago sana huuziwa watalii.
Soldiers of Tanzania People"s Defence Force (TPDF) stand beside the coffins of Tanzanian peacekeepers who were killed by by suspected Ugandan rebels, at the headquarters of Tanzania People"s Defence Force in Dar es Salaam on December 14, 2017. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Na Alhamisi, askari jeshi wa Tanzania wanatoa heshima zao za mwisho kwa wanajeshi 14 waliouawa wakilinda amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wiki iliyopita.
People wave Kenyan flags during the Independence Day ceremony, called Jamhuri Day ("Republic" in Swahili) at Kasarani stadium in Nairobi, Kenya, on December 12, 2017. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanamume huyu naye alikuwa miongoni mwa maelfu ya Wakenya waliojitokeza kwa sherehe za sikukuu ya Jamhuri, kuadhimisha kujinyakulia uhuru kwa taifa hilo kutoka kwa Uingereza.
Senegal"s President Macky Sall (L) and Japan"s Prime Minister Shinzo Abe (R) exchange national soccer jerseys at the end of a joint press conference at the Prime Minister"s official residence in Tokyo, Japan, 13 December 2017. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais wa Senegal Macky Sall na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe nao wanabadilishana jezi baada ya kumaliza kuwahutubia wanahabari kwa pamoja mjini Tokyo Jumatano.
This handout photo taken on December 9, 2017 by the Nigerian State House shows Nigerian President Muhammadu Bihari walking on his farm in Daura, Katsina State. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari naye anatembelea shamba lake nyumbani kwake Daura jimbo la Katsina.
In this handout image provided by the Spanish Royal Household Queen Letizia of Spain (2nd L) watches a performance during her visit on December 13, 2017 in Ziguinchor, Senegal Haki miliki ya picha EPA
Image caption Na Malkia Letizia wa Uhispania (pili kushoto) anawatazama watumbuizaji wa kitamaduni mjini Ziguinchor kusini mwa Senegal.
Khoisan Chief SA (C), Khoisan community members Christian Martin (L) and Brendon Willings (R) talk as they camp during the 12th day, outside the South African government "Union Buildings", in Pretoria on December 12, 2017. They were previously refused to enter the buildings by officials who complained about their traditional dress. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Na machifu hawa wa Khoisan walitembea kwa wiki mbili kutoka Port Elizabeth hadi Pretoria, na kupiga hema katika jumba la Union, makao makuu ya serikali, wakitaka kutambuliwa rasmi kwa lugha yao na pia jamii yao kama wakazi asili wa Afrika Kusini.

Picha kwa hisani ya AFP, EPA na Reuters

Mada zinazohusiana