Waathiriwa wa Thomas Lubanga DRC wapewa fidia na ICC

Thomas Lubanga akiwa ICC Desemba 2014 Haki miliki ya picha AFP/Getty

Majaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai wameagiza kulipwa fidia ya kitita cha dola milioni 10 kwa watoto waliotumikishwa kwenye jeshi na mbabe wa kivita wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Thomas Lubanga.

Hii ni mara ya kwanza ambapo mahakama hiyo ya ICC imeamuru watoto walipwe fidia.

Thomas Lubanga alihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela kwa kuwateka watoto wadogo, baadhi wakiwa na umri wa miaka 11.

Wavulana walilazimishwa kupigana katika eneo la Ituri mashariki mwa DRC.

Lubanga ahukumiwa miaka 14 Gerezani

Lubanga:'Nataka kusomea chanzo cha ukabila'

Wasichana walilazimishwa kuwa watumwa wa ngono.

Wakati wa kesi hiyo, mawakili walihoji iwapo inawezekana kujumlisha gharama ya maisha ambayo watoto hao walipokonywa.

Watoto wengi, wakiwemo wasichana waliorejea wakiwa na watoto wamekataliwa na jamii.

Ingawaje haijulikani jinsi dola milioni 10 zitakavyotumika, itagharimu watoto hao zaidi ya pesa hizo, kuuguza majeraha makubwa ya vita hivyo.

Mada zinazohusiana