Chama cha ANC cha Afrika Kusini kumchagua kiongozi mpya

Zuma anajiuzulu kama mwenyekiti wa ANC baada ya kuhudumu kwa muongo mmoja Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Zuma anajiuzulu kama mwenyekiti wa ANC baada ya kuhudumu kwa muongo mmoja

Chama cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini, kinatarajiwa kupiga kura kumchagua mrithi wa Rais Jacob Zuma kama kiongozi wake.

Wagombea wakuu ni makamu wa rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa, na waziri wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa rais Zuma.

Harakati hizo za kutafuta kiongozi zimezua mvutano chamani na kuna hofu kuwa huenda ANC kikagawanyika kabla ya uchaguzi wa mwaka 2019.

Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma anasema mustakabali wa chama tawala African National Congress upo katika tishio.

Alikuwa anazungumza katika mkutano wa kumchagua mtu atakayemrithi kama kiongozi wa chama hicho.

Rais Zuma alizungumza kuhusu haja ya kuwa na umoja ndani ya ANC, kinachotishiwa na kumeguka.

Mkutano huo ulichelewa kuanza kutokana na mizozo kuhusu nani anayestahili kuruhusiwa kupiga kura.

Zuma amesema tuhuma kuwa serikali yake ilishinikizwa na maslahi ya wafanya biashara zitachunguzwa.

Rais Jacob Zuma amekiongoza chama hicho kwa muongo mmoja sasa.

Chama hicho tawala kimekuwa kikipoteza umaarufu kutokana na kashfa za rushwa na tofuati za ndani ya chama chenyewe.

Lakini bado kina umaarufu katika ulingo wa kisiasa baad ya kuwepo madrakani kwa miaka 23.

Kikao hicho kinakutanaisha wajumbe takriban elfu tano mjini Johannesburg.

Wajumbe wanatarajiwa pia kuwachagua viongozi sita wa ngazi ya juu kuanzia rais wa chama hadi naibu katibu mkuu wa chama.

Haki miliki ya picha Reuters/AFP
Image caption Wagombea wakuu ni Nkosazana Dlamini-Zuma na Cyril Ramaphosa

Kivumbi hasa kipo katika Kinyanganyiro cha kumrithi rais Zuma, kama kiongozi wa chama- ni kati ya mkewe wa zamani Bi Nkosazana Dlamini-Zuma -- ambae pia aliwahi kuwa waziri na vilevile alikuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika.

Lakini anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wanaomuunga mkono makamu wa sasa Cyril Ramaphosa,

Mvutano huu pamoja na kashfa chungu nzima hasa za rushwa zinazomuandama rais Jacob Zuma zimeongoza hofu za kugawanyika kwa ANC.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa siku ya Jumapili.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii