Austria imerudi katika utawala wa mrengo wa kulia

Sebastian Kurz (kulia) and the Freedom Party's Heinz-Christian Strache reached a coalition deal Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sebastian Kurz (kulia) na Heinz-Christian Strache wa Freedom Party

Rais wa Austria, Alexander Van der Bellen ameidhinisha kuundwa serikali ya muungano kati ya chama cha kihafidhina People's Party na cha mrengo wa kulia Freedom Party.

Austria inaelekea kuwa nchi pekee ya Uropa magharibi kuwa na chama tawala kilicho na misimamo mikali ya mrengo wa kulia.

Hii inatokana na hatua ya kiongozi Sebastian Kurz wa chama cha conservative Austrian People's Party kuridhia ushirikiano na chama kidogo cha mrengo wa kulia Freedom Party kinachoongozwa na Heinz-Christian Strache, ambao wao wanaendeleza sera kali hasa dhidi ya wahamiaji.

Bwana Kurz mwenye ana miaka 31 pekee, na kama mpango huu utafanikiwa atakuwa pia kiongozi wa serikali mwenye umri mdogo zaidi duniani.

Kwa muda wa miezi miwili sasa bunge la nchi hiyo limekuwa likijadili vipi kuzuia uhamiaji nchini humo lakini maswali yanaulizwa - je hilo litaathiri vipi wa-Austria wanaotaka kuhamia mataifa mengine?

Vyama hivyo viliitawala nchi pamoja mwisho kati ya mwaka 2000 na 2005.

Viongozi hao wawili hawana taarifa kuhusu mpango wa serikali, lakini nyadhifa nyingi za uwaziri zinatarajiwa kukabidhiwa chama kidogo cha Freedom Party kama sehemu ya makubaliano.

Uchaguzi wa October 15 ulishindwa kutoa matokeo ya mwisho.

Kampeni iligubikwa kwa mzozo wa uhamiaji Ulaya, jambo ambalo chama kinachopinga uhamiaji cha Freedom Party kwa muda mrefu kimekuwa kikifanya kampeni kutumia suala hilo.

Kurz amewavutia wapiga kura wa kihafidhina na wa mrengo wa kulia kwa ahadi zake za kufunga njia wanaozpitia wahamiaji kuingia Ulaya, kupunguza malipo kwa wakimbizi , na kuwazuia wahamiaji kupokea malipo hadi pale watakapokuwa wamishia Austria kwa zaidi ya miaka mitano.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii