Aanguka kutoka orofa ya 62 na kufariki

Wu alijulikana kama "rooftopper" akining'inia kutoka orofa kama anavyoonekana hapa Haki miliki ya picha WEIBO
Image caption Wu alijulikana kama "rooftopper" akining'inia kutoka orofa kama anavyoonekana hapa

Mwezi uliopita, Wu Yongning alielekea kufanya anachopenda kufanya - kuparaga orofa za majengo makubwa bila ya vifaa vyovyote vya usalama na hujipiga video akining'inia kutoka juu ya mjengo huo kwa vidole vyake tu vya mkononi.

Kilichofuata baada ya hapo pengine sio jambo la kushtusha - raia huyo wa Kichina alianguka orofa 62 kutoka juu na kufariki papo hapo.

Maelfu ya wafuasi wake walishikwa na wasiwasi alipoacha kuweka video za vituko vyake katika mitandao kama vile Huoshan na Kuaishou, lakini kifo chake kilithibitishwa katika siku chache tu za hivi karibuni, kwanza na mpenzi wake baadaye likafuata tanagzo la kmaafisa wa utawala.

Kanda ya video ya kushtusha ya kilichoonekana kuwa muda wake wa mwisho wa uhai - jaribio lake la kuparaga kuta za orofa hiyo katika mji wa Changsha city - ilianza kusambaa katika mtandao wiki hii.

Kifo chake kimezusha maswali mengi ya wasiwasi na ya kutafakari kuhusu kuhatarisha maisha katika kutafuta pesa "cash for clips" sekta ya kusambaza video za aina hiyo katika mitandao.

Maswali sasa yanaulizwa, kuhusu iwapo majukwaa haya katika mitandao na watazamaji wake ndiyo yanayohusika kwa kifo chake.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii