Familia yenye watu wasiohisi maumivu

Mara nyingi hawatambui mifupa yao inapovunjika au wanapoteketea moto kutokana na kutosikia maumivu, hivyobasi hawapoi vizuri Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mara nyingi hawatambui mifupa yao inapovunjika au wanapoteketea moto kutokana na kutosikia maumivu, hivyobasi hawapoi vizuri

Letizia Marsili, mwenye umri wa miaka 52, alitambua kwamba yuko tofauti kwa mara ya kwanza alipokuwa mdogo.

Hakuhisi maumivu kwa haraka, jambo linalomaanisha kwamba hakuhisi alipokuwa anateketea, au kutambua kwamba amevunjika mfupa mwilini. Jamaa zake watano pia katika familioa yao pia walikuwa katika hali hiyo na hawakuhisi maumivu.

Letizia ameiambia BBC: "siku hata siku tunaishi maisha ya kawaida, pengine maisha bora kuliko watu wengine, kwasababu ni aghalabu sisi kuwa wagonjwa, na hatuhisia maumivu.

"Hatahivyo, ki ukweli, maumivu yapo ila ni wa sekundi chache tu."

Wanasayansi wanaamini hali hii huenda inatokana na kutofanya kazi vizuri kwa baadhi ya neva mwilini.

RWatafiti walioikagua familia hiyo wanatarajiwa kuwa uchunguzi wao utasaidia watu wanaogua mamuivu makubwa katika siku zijazo.

"Tumefungua njia mpya kwa uvumbuzi wa dawa za maumivu," amesema Prof Anna Maria Aloisi kutoka chuo kikuu cha Siena nchini Italia.

Haki miliki ya picha Letizia Marsili
Image caption Letizia Marsili ana jamaa zake watano aghlabu huhisi uchungu

Ni kwanini wanahisi uchungu mdogo?

Kiongozi wa watafiti Dr James Cox, kutoka University College London, amesema familia hiyo zina neva mwilini, lakini "hazifanyi kazi zinavyostahili".

Amesema: "TUnashughulika kupata uelewa zaidi wa kwanini hasaa hawahisi maumivu, kuona iwapo hilo litatusaidia kuvumbua dawa mpya za maumivu."

Utafiti wa wataalamu hao ambao umechapishwa katika jarida la Brain, zilishirikiana na familia kujua ni vyenzo gani vilivyounda Jini zao mwilini.

Marsili syndrome, hali hiyo iliyopewa jina la familia hiyo, inamaanisha kwamba mtu huhisi kwa kiwango kidogo mno cha joto, kuwashwana pilipili na hawahishi maumivu mifupa yao inapovunjika mwilini tofuati na watu wengine.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii