Wito watolewa kuharakisha kuuawa wabakaji India

Bi Maliwal amesema kuna uelewa mzuri zaidi kuhusu visa vya ubakaji - lakini hilo halijatatua matatizo ya ubakaji India Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bi Maliwal amesema kuna uelewa mzuri zaidi kuhusu visa vya ubakaji - lakini hilo halijatatua matatizo ya ubakaji India

Wabakaji wa watoto wanapaswa kuuawa katika muda wa miezi sita tangu watekeleza uovu huo, mteteaji mkuu wa haki za wanawake India amependekeza.

Swati Maliwal ametoa ombi hilo katika barua aliyomuandikia waziri mkuu Narendra Modi.

Iliandikwa kuendana na kumbukumbu ya mwaka wa tano tangu mwanafunzi Jyoti Singh mwenye umri wa miaka 23 alipobakwa na gengi la wanaume, kifo chake kilichozusha maandamano ya kitaifa.

"Hakuna kilichobadilika kaika miaka mitano iliyopita," Bi Maliwal, ameiambia BBC.

"Delhi bado ndio mji mkuu wa ubakaji. Mwezi uliopita, mtoto wa kike wa mwaka mmoja na nusu alibakwa na gengi la wanaume, na ubakaji wa mtoto wa miaka saba,na mwingine wa kike wa mwaka mmoja na nusu alibakwa."

Kwa wastani, alisema, watoto watatu wa kike na wanawake wasita wanabakwa katika mji mkuu huo kila siku.

India ilifanyia mageuzi sheria zake kuhusu ubakaji kutokana na shutuma miaka mitano iliopita, na ilichukua hatua kuharakisha kusikilizwa kesi na kuwashinikiza maafisa wa polisi kutilia uzito tuhuma za ubakaji na unyanyasaji wa kingono.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii