Shambulizi baya latokea kwenye kanisa Pakistan

A bearded man carries a girl, dressed in white, from the scene of the attack Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shambulizi baya latokea kwenye kanisa Pakistan

Mlipuaji wa kujitoa mhanga na shambulizi la bunduki katika kanisa la Methodist huko Pakistan yamesababisha vifo vya takriban watu watano.

Shambulizi hilo lilitokea kwenye mji wa Quetta kilomita 65 kutoka mpaka na Afghanistan.

Zaidi ya watu 10 pia walijeruhiwa baada ya watu wenye bundukia waliokuwa wamejifunga milipuko kujaribu kuingia jengo hilo.

Washambuliaji hao walizuiwa kwenye lango la jengo la kanisa.

Isingekuwa watu watu hao walizuiwa kuingia kungekuwa na vifo vya mamia ya watu, waziri wa masuala ya nyumba eneo hilo alisema.

Image caption Shambulizi baya latokea kwenye kanisa Pakistan

Mwanamume mmoja alilipua milipuko yake na mwingine akazuiwa wakati wa ufyatullianaji wa risasi na polisi.

Vikosi vya usalama vinafanya msako na wamelizingira eneo hilo.

Mashambulizi kama hayo eneo hilo lemye wasunni wengi ni ya kawaida na mara nyingi yamelenga jamii ya washia wa Hazara.

Lakini jamii ndogo ya wakiristo nchini Pakistan wamelengwa na wanamgambo na kuchangia walinzi kuwekwa karibu na kanisa eneo la Quetta.

Mada zinazohusiana