Je,ni sahihi kwa Suu Kyi kufunguliwa mashitaka ya mauaji ya kimbari

kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi
Image caption kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi

Mkuu wa Shirika la haki za binadamu la umoja wa mataifa ameiambia BBC kuwa anadhani kwamba kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi amekuwa akitetea ukandamizaji wa jamii ndogo ya watu wa Rohngya. Zeid Ra'ad Al Hussein amesema kuwa ni sahihi kwa kiongozi huyo afunguliwe mashitaka ya mauaji ya kimbari.

"Hicho tunachokisema kinalingana na kile tunachoona,tunahisi kuwa huwezi kutenganisha. ,swali ambalo mataifa yanarejea la mauji ya kimbari ambayo yalifanyika, Ni ngumu sana kuelezea tatizo lilivyo kwa kuwa kuna vipingamizi vingi na ndio maana tunafahamu kwamba kuendelea kusema kuwa mahakama inapaswa kufanya hiki na hiki lakini hilo halitanishangaza kama siku za usoni mahakama itatoa hukumu kwa kile tunachokiona.''

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption wakazi wa Rohngya

Aidha Zeid Ra'ad Al Hussein amesema yeye mwenyewe binafsi aliwahi kumuomba kiongozi wa Mynmar kuachana na ukatili ambao alikuwa akiufanya.Kiongozi anasema aliwahi kuongea na Aung San Suu Kyi kwenye simu na kumuomba asitishe majeshi yake katika mapigano na kwa masikitiko makubwa hakuona chochote kikifanyika.

Hivyo akasema kuwa hili ni jambo baya sana ,ni muhimu kuliangalia,ila baada ya siku chache baada ya kuuliza njia tulizotumia ,walianza kuuliza kama huo ndio ukweli.

Mada zinazohusiana