Picha za wanyama za kuchekesha zaidi 2017

Happy Sea Otter Haki miliki ya picha Penny Palmer/ Barcroft Images

Huu hapa ni mkusanyiko wa picha za kuchekesha na kusisimua za wanyama zilizopigwa mwaka huu, miongoni mwa picha hizi ikiwa moja ya dubu wanaoonekana kukoleza uhusiano wao pamoja na nyingine ya sili.

Picha hizi ziliteuliwa kushindania tuzo za picha za ucheshi za wanyama mwaka huu, katika vitengo vitano.

Jumla ya picha 3,500 ziliwasilishwa kwa mashindano hayo.

Shindano hili huandaliwa kuchangisha pesa na kusaidia shirika la kutetea uhifadhi wa wanyama la Wakfu wa Born Free.

Haki miliki ya picha Tibor Kercz/ Barcroft images
Image caption Picha hii ya Tibor Kercz ilipewa kichwa 'Nisaidie'

Mshindi wa jumla Tibor Kercz kwa picha hii yake ya bundi anayeonekana kuhitaji usaidizi kujishikilia vyema kwenye tawi mti alitunukiwa kikombe ambacho kilitengenezwa na wanaume na wanawake wenye ulemavu kutoka Tanzania.

Kadhalika, alipewa vifaa zaidi vya kupigia picha.

Alishinda pia tuzo kwenye kitengo cha picha ya kuvutia zaidi ya mtandaoni pamoja na kujishindia safari ya kwenda mbugani Kenya.

Kabla ya picha hii ya Andrea Zampatti kushinda kitengo cha picha za ardhini, picha hii yake ya panya anayeonekana kuangua kicheko ilisambazwa sana mitandao ya kijamii mapema mwaka huu.

Haki miliki ya picha Andrea Zampatti /Barcroft Images
Image caption Raha mustarehe!

Na ingawa bahari ni kubwa, picha hii iliyoshinda kitengo cha picha za chini ya bahari inaonesha viumbe wanaweza bado kukaribiana sana.

Haki miliki ya picha Troy Mayne/ Barcroft Images
Image caption Picha hii ilipewa kichwa 'kofi'

Kitengo cha picha za angani, picha hii ya njiwa mmoja wao akionekana kufuata njia ya moshi wa ndege, iliyopigwa na John Threlfal Preston, Lancashire ndiyo iliyoshinda.

Haki miliki ya picha John Threlfal/ Barcroft Media

Hapa chini ni baadhi ya picha nyingine zilizofanya vyema.

Haki miliki ya picha Carl Henry/ Barcroft Images
Image caption Twende kanisani
Haki miliki ya picha Olivier Colle/ Barcroft Images
Image caption Kunani?
Haki miliki ya picha Daisy Gilardini/ Barcroft Media
Image caption Nibebe
Haki miliki ya picha Jean-Jacques Alcalay/ Barcroft Images
Haki miliki ya picha Bence Mate/ Barcroft Images
Image caption Mapenzi tele
Haki miliki ya picha George Cathcart/ Barcroft Images
Image caption Eti nini!?

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii