Serena Williams adai kusumbuliwa na mtoto

Serena Williams na Alexis Ohanian Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Serena Williams na Alexis Ohanian

Nyota wa tennis Serena Williams adai kuwa anasumbuliwa sana na mtoto. Anasema kuwa mto huyo msichana, Alexis Olympia, wa umri wa miezi mitatu unusu amekuwa akilia anapomea meno.

Anasema alilazimika kumshika mikononi mwake hadi wakati alilala, baada njia zote alizojaribu kutumia kumtuliza kushindikana.

Hivi majuzi Serena Williams alifunga ndoa na mwanzilishi mwenza wa Reddit Alexis Ohanian katika harusi kubwa iliojaa mbwembwe za aina yake ya mwaka huu.

Nyota akiwemo Beyonce, Kim Kardashian na Eva Longoria walikuwa katika harusi hiyo iliofanyika katika eneo la New Orleans siku ya Alhamisi.

Sherehe hiyo ilikuwa na wageni 200 katika orodha ya wageni kulingana na vyombo vya habari.

Eneo moja kubwa la mji lilifungwa kwa sherehe hiyo ambayo ilifanyika katika kituo cha Contemporary Arts Center.

Mada zinazohusiana