Manowari mpya ya Uingereza ya kubeba ndege yagunduliwa kuwa na hitilafu

HMS Queen Elizabeth Haki miliki ya picha PA
Image caption Manowari mpya ya kubeba ndege ya Uingereza HMS Queen Elizabeth, inavuja kutokana na hitilafu iliyo nayo

Manowari mpya ya kubeba ndege ya Uingereza HMS Queen Elizabeth, inavuja kutokana na hitilafu iliyo nayo.

Manowari hiyo iliyozinduliwa rasmi na malkia mapema mwezi huu huko Portsmouth, ina hitilafu katika mitambo yake ya chini.

Hitilafu kwenye manowari hiyo iliyogharimu pauni bilioni 3.1 kujengwa iligunduliwa mara ya ikifanyiwa majaribio baharini.

Msemaji wa jeshi la wanamaji nchini Uingereza alisema manowari hiyo itafanyiwa ukabati na hitilafu hiyo haitaizuia kuendelea na majaribio mapema mwaka ujao.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Manowari hiyo ilizinduliwa rasmi na malkia mapema mwezi huu huko Portsmouth

Swali sasa ni ikiwa hitilafu hiyo itarekebishwa manowari hiyo ikiwa tayari baharini.

Jeshi linasisitiza kuwa kazi hiyo inaweza kufanywa bila na manowari hiyo kurudishwa kwenye kiwanda.

Manowari hiyo ya urefu wa mita 280 ilifika eneo lake la kuegeshwa kwa mara ya kwanza mwezi Agosti baada ya kuanza majaribio ya baharini ya miezi miwili ikitokea Rosyth dockyard ambapo ilijengwa.

Ni manowari ya kwanza kabisa ya aina yake ya kubeba ndege kujengwa na Uingereza.

Mada zinazohusiana